TEHRAN : Mripuko mwengine katika mji wa Zehadan | Habari za Ulimwengu | DW | 17.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN : Mripuko mwengine katika mji wa Zehadan

Shirika la habari la serikali nchini Iran IRNA limeripoti kutokea mripuko mwengine katika mji wa kusini mashariki wa Zehadan ikiwa ni masaa machache tu baada ya mazishi ya wanajeshi 11 wa Kikosi cha Mapinduzi cha Iran ambao waliuwawa katika mripuko kwenye mji huo hapo Jumaatano.

Katika tukio hilo la hivi karibuni kabisa IRNA imesema waasi waliripuwa bomu hilo la kishindo ambalo halikusababisha madhara yoyote yale.

Zehadan iko katika eneo la Iran karibu na mipaka na Afghanistan na Pakistan ambako kuna jamii ya Wabaluchi, Waislamu wa madhehebu ya Sunni walio wachache.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com