TEHRAN: Miripuko kadhaa yasikika katika ubalozi wa Uingereza | Habari za Ulimwengu | DW | 01.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN: Miripuko kadhaa yasikika katika ubalozi wa Uingereza

Miripuko imesikika ndani ya ubalozi wa Uingereza mjini Tehran hii leo. Walioshuhudia wanasema moshi mweusi ulionekana ukitoka ndani ya ubalozi huo katikati mwa mji mkuu Tehran wakati wa maandamano kuhusu mabaharia saba na wanajeshi wanane wa Uingereza wanaozuiliwa na Iran. Hakuna aliyejeruhiwa katika maandamano hayo.

Mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo amesema miripuko minane imesikika baada ya mabomu ya petroli kuvurumishwa katika uwanja wa ubalozi wa Uingereza mjini Tehran.

Uingereza imethibitisha kwamba hakuna uharibifu wowote uliosababishwa na mabomu hayo katika ubalozi wake na hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Wanafunzi takriban 200 walifanya maandamano ya fujo nje ya ubalozi wa Uingereza huku wakirusha mawe, lakini polisi wakawazuilia kuingia ndani ya ubalozi huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com