Suala la Zimbabwe lajadiliwa katika mkutano maalum wa umoja wa mataifa | Matukio ya Kisiasa | DW | 17.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Suala la Zimbabwe lajadiliwa katika mkutano maalum wa umoja wa mataifa

Mkutano wa Umoja wa mataifa kuhusu Afrika haujasaidia kuupatia ufumbuzi mzozo wa Zimbabwe

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe

Rais Robert Mugabe wa ZimbabweMacho ya upande wa upinzani nchini Zimb abwe yalikodolewa kwa hamu kubwa mjini New-York hapo jana.Walitaraji mkutano wa kilele wa baraza la usalama ungebadilisha mkondo wa mambo baada ya uchaguzi nchini Zimbabwe.Kwasababu wiki tatu baadae ,bado mshindi wa uchaguzi huo hajulikani.Na nchi jirani hazifanyi vya kutosha kumaliza mzozo huo.


Rais Thabo Mbeki wa Afrika kusini amelikwepa maksudi suala hilo.Katika hotuba yake ya ufunguzi,kama mwenyekiti wa mkutano huo wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusu Afrika,rais Mbeki amezungumzia kwa muda mrefu kuhusu matatizo ya kugharimia shughuli za kulinda amani barani humo.Mzozo wa Zimbabwe hakuutaja hata mara moja

.

Kimsingi, Thabo Mbeki ndie aliyekua ametwikwa jukumu muhimu kuhusu suala hilo hata kabla ya mkutano huo kuanza. Rama yade katibu wa dola katika wizara ya mambo ya nchi za nje ya Ufaransa anaeshughulikia masuala ya haki za binaadam anasema:


""Tunaihitaji Afrika kusini,ikiwa tunataka kupata ufumbuzi wa eneo hilo."


Hakua peke yake aliyezungumzia hofu kuhusu hali ya mambo nchini Zimbabwe.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amekumbusha madhara yanayoweza kuwakumba wananchi nchinih umo na kitisho cha kuingia dowa utaratibu wa kueneza kidemokrasia barani Afrika.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon anataka wasimamizi huru wa uchaguzi wapelekwe nchini Zimbabwe.


"Ushirikiano wetu wakati wa mzozo wa Kenya ni ushahidi unaonyesha tunaweza kufanikiwa pakubwa tukishirikiana."


Wawakilishi wa Afrika waliohudhuria mkutano huo hawakuwa na hamu kubwa ya kulishughulikia suala la Zimbabwe.


Matamshi makali lakini yametolewa na waziri mkuu wa Uengereza Gordon Brown."Hakuna yeyote anaeamini kwa dhati kwamba Robert Mugabe ameshinda uchaguzi" amesema Gordon Brown na kushadidia:


"Uchaguzi wa wizi si uchaguzi wa kidemokrasi."


Muakilishi maalum wa Marekani katika Umoja wa mataifa,Zalmay Khalilzad amehamakishwa sana na jinsi wawakilishi wa Afrika walivyoonyesha hawana hamu ya kuzungumzia mzozo wa Zimbabwe.


"Huezi kuitisha mkutano kuhusu Afrika bila ya kuzungumzia mzozo unaoendelea hivi sasa nchini Zimbabwe."


Wananchi walio wengi wamepiga kura kudai mageuzi-anasema Khalilzad.Ndio maana ni jukumu la Umoja wa mataifa kutuma ujumbe nchini Zimbabwer,ili,kama balozi nhuyo wa Umoja wa mataifa anavyosema-kulifikia lengo hilo."


Zimbabwe na majirani zake wanashikilia kuupatia wenyewe mzozo ulioko.Hasa Afrika kusini,imekua kila kwa mara ikijitokeza kama mlinzi wa rais Robert Mugabe.Hata hivyo rais Mbeki anasema:


"Kama kuna kosa,nnajua kuna kosa.Ile hali kwamba mie mwenyewe nnatokana na vuguvugu la ukombozi wa Afrika,haimaanishi kwamba sitambui kama makosa yamefanyika."


Hilo lilikua jibu la mwisho la rais Mbeki katika mkutano pamoja na waandishi habari.Dhana lakini ziko pale pale.

 • Tarehe 17.04.2008
 • Mwandishi Schmidt, Thomas / New York (WDR)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Djc0
 • Tarehe 17.04.2008
 • Mwandishi Schmidt, Thomas / New York (WDR)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Djc0
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com