Steinmeier aunga mkono wito wa kuhesabu upya kura. | Habari za Ulimwengu | DW | 04.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Steinmeier aunga mkono wito wa kuhesabu upya kura.

Berlin. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameunga mkono wito wa kufanyika uchunguzi juu ya mvutano wa matokeo ya uchaguzi nchini Kenya. Katika taarifa , Steinmeier amesema kuwa anaunga mkono wito uliotolewa na mwanasheria mkuu wa serikali ya Kenya mjini Nairobi pamoja na kundi la wachunguzi wa uchaguzi la umoja wa Ulaya la kutaka kuhesabiwa tena kwa kura. Hesabu mpya ya kura amesema , inaweza kuweka msingi wa maridhiano baina ya vyama na makabila na kuirejesha Kenya katika njia ya demokrasia. Ujerumani inaunga mkono juhudi za kimataifa kuingilia kati mzozo huo, hususan kwa upande wa umoja wa Afrika na kutoa wito kwa serikali na upande wa upinzani kuepuka uchochezi na ghasia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com