SOFIA : Wanatiba wa kigeni wamesema wameteswa Libya | Habari za Ulimwengu | DW | 11.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SOFIA : Wanatiba wa kigeni wamesema wameteswa Libya

Wauguzi wa Bulgaria wametowa ushahidi mjini Sofia dhidi ya askari wa magereza wa Libya ambao wanasema waliwatesa kuwalazimisha wakiri kwamba waliwaambukiza kwa makusudi virusi vya HIV na UKIMWI mamia ya watoto wa Libya.

Waendesha mashtaka wa Bulgaria wanapanga kuwafikisha wanamagereza hao wa Libya mahkamani iwapo utapatikana ushahidi wa kutosha.Waaguzi hao watano na daktari mmoja wa Kipalestina ambaye hivi sasa ana uraia wa Bulgaria waliachiliwa uhuru mwezi uliopita chini ya makubaliano ya ushirikiano kati ya Libya na Umoja wa Ulaya baada ya kusota gerezani kwa miaka minane nchini Libya.Wote sote walikuwa wakisisitiza kwamba walikuwa hawana hatia.

Hapo Alhamisi mwana wa kiume wa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi alikiri kwamba wanatiba hao wa kigeni waliteswa wakati walipokuwa mahabusu nchini Libya.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com