Silaha za nyuklia katika mataifa ya NATO | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 15.10.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Silaha za nyuklia katika mataifa ya NATO

Ujerumani yapiga kampeini ya kuachana na silaha za nyuklia.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Karl-Theodor zu Guttenberg na mwenzake wa mambo ya nje Guido Westerwelle, wakiwa mjini Brussels.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Karl-Theodor zu Guttenberg na mwenzake wa mambo ya nje Guido Westerwelle, wakiwa mjini Brussels.

Ujerumani na Ufaransa zimetofautiana kuhusiana na kuwepo kwa silaha za nyuklia katika mataifa wanachama wa Jumuiya ya kujihami ya NATO. Mawaziri wa Ulinzi pamoja wa Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa 28 ya Jumuiya hiyo, wanakutana mjini Brussels kuzungumzia azimio la mkakati mpya wa ulinzi. Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle na mwenzake wa Ulinzi Karl-Theodor Zu Guttenberg walisema suala la kuachana na silaha za nyuklia linafaa kuwepo katika mkakati huo mpya. Pia walisema nchi kadhaa zinaunga mkono msimamo huo wao. Lakini Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Herve Morin alipinga msimamo huo. Alishikilia kuwa Jumuiya hiyo ya NATO bado inahitaji kuwa na mfumo wa kujihami kutokana na silaha za nyuklia, msimamo ulioungwa mkono na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates. Mkakati huo mpya wa NATO utapitishwa katika mkutano wa utakaofanyika wiki ijaayo, mjini Lisbon Ureno.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com