Shambulio la mzinga lauwa wanane Mogadishu | Habari za Ulimwengu | DW | 31.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Shambulio la mzinga lauwa wanane Mogadishu

MOGADISHU

Shambulio la mzinga limeuwa watu wanane wa familia moja kwenye kambi ya wakimbizi mjini Mogadishu.

Huo ni umwagaji damu mpya katika mji mkuu wa Mogadishu kati ya waasi wa itikadi kali za Kiislam na wanajeshi wa serikali ya mpito ya nchi hiyo.Katika tukio jengine tafauti waasi pia wamepambana na wanajeshi kusini mwa mji mkuu huo na pia wamewashambulia wanajeshi wa kulinda amani wa Uganda wanaolinda kiungo muhimu cha mji mkuu huo.

Vikosi vya Ethiopia vilianza kuisaidia serikali ya mpito ya Somalia mwaka mmoja uliopita na kutokomeza mara moja wanamgambo wa Kiislam ambao kwa muda mfupi walikuwa wakidhibiti sehemu kubwa kusini mwa nchi hiyo na katikati mwa nchi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com