SERBIA- KOSOVO.Mjumbe maalum wa UM awasilisha pendekezo | Habari za Ulimwengu | DW | 02.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SERBIA- KOSOVO.Mjumbe maalum wa UM awasilisha pendekezo

Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa Martti Ahtissari amezindua mswaada unaohusu hali ya baadae ya jimbo lililojitenga la Serbia,Kosovo.

Nia hasa ya pendekezo hilo ni kutafuta njia ya kulifanya jimbo hilo litambulike kama taifa chini ya usimamizi wa umoja wa mataifa.

Lakini pendekezo hilo halizungumzii juu ya uhuru wa Kosovo.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Belgrade Ahtassari amesema kuwa pande hizo mbili hasimu wa -Serbia na wakosovo wenye asili ya Albania wanabidi wakutane tena kwa mazungumzo yenye lengo la kusaka maridhiano.

Rais wa serbia Boris tadic hata hivyo amelikatalia mbali pendekezo hilo la umoja wa mataifa, amesema kamwe hatautambua uhuru wa jimbo lililojitenga

Ahtassari anatarajiwa pia kwenda Prishtina kuwasilisha mpango wake huo kwa viongozi wa Kosovo wenye asili ya Albania.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com