1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yaimarisha ukaguzi wa kiafya mpakani

1 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVZ9

Maafisa nchini Rwanda wamesema,ukaguzi wa kiafya umeimarishwa kwenye mpaka wake,ili kuzuia usambazaji wa aina mpya ya virusi vya homa ya Ebola kutoka magharibi mwa Uganda.Afisa wa afya nchini Rwanda,Innocent Nyaruhirira amesema, serikali ina wasi wasi kwa sababu eneo hilo lipo karibu na vile vile kuna harakati nyingi za kibiashara na kijamii katika eneo hilo la mpakani.