ROSTOCK: Bush amewasili kuhudhuria mkutano wa G8 | Habari za Ulimwengu | DW | 06.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ROSTOCK: Bush amewasili kuhudhuria mkutano wa G8

Rais George W Bush wa Marekani amewasili katika mji wa mashariki wa Rostock kuhudhuria mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi nane zilizostawi kiviwanda G8.

Mkutano huo unatarajiwa kuanza hii leo katika mji wa pwani wa Heiligendamm.

Bush amewasili hapa nchini Ujerumani akitokea Prague mji mkuu wa Jamuhuri ya Czech alikofanya mazungumzo na rais Vaclav Klaus pamoja na waziri wake mkuu Mirek Topolanek.

Akihutubia kikao cha demokrasia na maswala ya usalama mjini Prague rais Bush alimshutumu rais Vladmir Puttin wa Urusi na kutaja kuwa harakati za marekebisho ya demokrasia nchini humo zimekwama.

Rais Bush na rais Puttin watakuwa na mazungumzo ya pande mbili pembezoni mwa mkutano wa wakuu wa nchi za G8.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com