RAMALLAH: Viongozi wa Palestina washindwa kuafikiana juu ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa | Habari za Ulimwengu | DW | 07.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RAMALLAH: Viongozi wa Palestina washindwa kuafikiana juu ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa

Rais wa Palestina, Mahmud Abbas kutoka chama cha Fatah na waziri wake mkuu, Ismail Haniya kutoka chama cha Hamas,walishindwa kuondoa tofauti zao kuhusu uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa. Miongoni mwa matatizo yaliojitokeza ni pamoja na nani ataiongoza serikali hiyo iwapo itaundwa. Viongozi hao wawili wanatarajiwa kukutana tena leo kwa mazungumzo zaidi juu ya swala hilo.

Wakati hayo yakiarifiwa, majeshi ya Israeli yameondoka kutoka mji wa kaskazini mwa ukanda wa Gaza wa Beit Hanun baada ya operesheni ya wiki nzima ambapo kwa uchache wapalestina 50 waliuawa na mia kadhaa kujeruhiwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com