Ramallah. Serikali ya umoja wa kitaifa kuundwa hivi karibuni. | Habari za Ulimwengu | DW | 12.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ramallah. Serikali ya umoja wa kitaifa kuundwa hivi karibuni.

Rais wa mamlaka ya palestina Mahmoud Abbas amesema kuwa anaimani kuwa serikali ya umoja wa kitaifa itakayokuwa na wajumbe kutoka katika makundi ya wapiganaji ya Hamas na Fatah inawezekana kuundwa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

Abbas ametoa taarifa hiyo katika mji wa Ramallah , katika hotuba kuadhimisha mwaka wa pili wa kifo cha mtangulizi wake Yasser Arafat.

Marekani na mataifa ya Ulaya yameweka vikwazo vinavyoiathiri nchi hiyo dhidi ya mamlaka ya Wapalestina baada ya chama cha Hamas kukishinda chama cha Fatah katika uchaguzi wa bunge mwezi wa Januari. Pande hizo mbili zinamatumaini kuwa uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa utazishawishi nchi za magharibi kuacha mgomo wake wa kutoa misaada kwa Palestina.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com