RAMALLAH: Mwanamgambo wa Fatah ameuawa Ukanda wa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 22.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RAMALLAH: Mwanamgambo wa Fatah ameuawa Ukanda wa Gaza

Watu wenye bunduki walioficha nyuso zao,wamemuua mwanamgambo wa ngazi ya juu wa Fatah katika kambi ya wakimbizi kwenye Ukanda wa Gaza.Maafisa wa Fatah wameviweka vikosi vyake katika hali ya tahadhari na wamekilaumu chama cha itikadi kali cha Hamas kwa shambulio hilo.Mwezi huu,hadi Wapalestina 19 wameuawa katika mapigano ya ndani na kuna hofu ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe.Kwa upande mwingine,katika mkutano uliofanywa siku ya Jumamosi,waziri mkuu wa Wapalestina Ismail Haniyeh alishauriwa na Wapalestina wa ngazi ya juu afikirie kuunda baraza la mawaziri lenye wasomi na hivyo kuumaliza mgogoro wake na chama cha Fatah unaohusika na suala la kuunda serikali ya umoja.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com