Raia wawili wa Ivory Coast apigwa risasi | Habari za Ulimwengu | DW | 31.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Raia wawili wa Ivory Coast apigwa risasi

Maafisa wa usalama nchini Misri wamewapiga risasi na kuwaua raia wawili wa Ivory Coast waliokuwa wakijaribu kuvuka mpaka na kuingia Israel kinyume cha sheria hapo jana.

Mwanamume mwenye umri wa miaka 22 na mwanamke wa miaka 18 walipigwa risasi wakati walipokataa kutii amri ya polisi kuwakata wasimame kilomita 30 kusini mwa kivuko cha mpakani cha Rafah.

Mwanamke huyo alipigwa risasi tumboni na mguuni huku mwanamume akipigwa risasi kwenye paja. Wote wawili walivuja damu hadi wakafa kabla gari la kubebea wagonjwa kufika katika eneo hilo la mpakani.

Raia sita wa Eritrea na Waethiopia wawili waliokuwa wakisafiri pamoja na raia hao wawili wa Ivory Coast walikamatwa na sasa wanahojiwa na polisi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com