Raia wa Sudan Kusini warejea nyumbani | Matukio ya Afrika | DW | 21.12.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Raia wa Sudan Kusini warejea nyumbani

Ni katika juhudi ya kujiandaa kushiriki katika kura itakayoamua kama Sudan kusini ijitenge na utawala wa Khartoum ama la

Kiasi ya Wasudan kusini 55,000 waliolazimika kuyahama makaazi yao wakati wa vita, wamerejea kutoka upande wa kaskazini katika wiki za hivi karibu. Kwa mujibu wa Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa, wakaazi hao wanarejea kusini tayari kupiga kura ya maoni mwezi ujao juu ya mustakbali wa eneo hilo. Sudan kusini itaamua kama inataka kujitenga na kaskazini au kubakia kama sehemu ya Sudan moja.