Raia wa kigeni waikimbia Libya | Matukio ya Kisiasa | DW | 24.02.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Raia wa kigeni waikimbia Libya

Hali nchini Libya imeendelea kuwa ya wasi wasi,wakati kiongozi wa nchi hiyo kanali Muammar Gaddafi akijaribu kurejesha udhibiti wa mji mkuu Tripoli na maeneo ya magharibi.

default

Waandamanaji wakibeba mabango na kuimba kauli mbiu za kumshutumu kanali Gaddafi

Hali nchini Libya imeendelea kuwa ya wasi wasi wakati kiongozi wa nchi hiyo kanali Muammar Gaddafi akijaribu kurejesha udhibiti wa mji mkuu Tripoli pamoja na maeneo ya magharibi. Mashariki mwa nchi hiyo, wanajeshi wa serikali wameamua kuunga mkono upande wa upinzani na wamejiunga na waandamanaji ambao wamechukua udhibiti wa eneo hilo.

Süd-Koreas Außenminister Ban Ki-moon ist Kandidat für das Amt des UN-Generalsekretärs

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa , Ban Ki-moon , amesema kuwa anaangalia matukio katika nchi hiyo kwa wasi wasi mkubwa. Wakati huo huo, umoja wa Ulaya na Marekani zimeshutumu ghasia hizo zinazoendelea ambazo zimesababisha watu karibu 300 kuuwawa. maelfu ya raia wa kigeni wanajaribu kuikimbia nchi hiyo kwa njia zozote zinazopatikana. Jana Jumatano jioni , ndege mbili za Ujerumani ziliwasili katika viwanja vya ndege vya Frankfurt na Kolon kutoka Tripoli zikiwa na idadi kadha ya Wajerumani ambayo haikutajwa, pamoja na raia wengine wa mataifa ya Ulaya.

 • Tarehe 24.02.2011
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/10Oah
 • Tarehe 24.02.2011
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/10Oah

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com