POTSDAM : Watuhumiwa wa shambulio wako huru | Habari za Ulimwengu | DW | 15.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

POTSDAM : Watuhumiwa wa shambulio wako huru

Wajerumani wawili wanaotuhumiwa kumpiga Muethiopia mzalia wa Ujerumani Ermyas Mulugeta katika shambulio la kigaidi karibu na Berlin wameonekana kuwa hawana hatia.

Katika hukumu iliotolewa na mahkama mjini Potsdam mahakimu wameona kwamba hakuna ushahidi kuthibitisha kwamba watuhumiwa hao wawili walihusika na kipigo cha mtu huyo.

Hata hivyo Thomas Zippel wakili wa Mulugeta alikuwa anaamini kwamba shambulio hilo sio tu ni ugomvi uliochochewa na ulevi bali ni uhalifu unaotokana na chuki.

Shambulio hilo la mwezi wa April mwaka jana lilimwacha muhanga huyo aliepigwa Mulugeta bila ya fahamu kwa wiki kadhaa.

Amesema alikuwa akimpigia simu mke wake wakati shambulio hilo lilipotokea na kwamba washambuliaji wake walirekodiwa sauti zao kwenye simu ya mke wake wakati wakimkejeli kwa matusi ya kibaguzi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com