PORT-AU-PRINCE: Walinzi wa amani wameuawa nchini Haiti | Habari za Ulimwengu | DW | 12.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PORT-AU-PRINCE: Walinzi wa amani wameuawa nchini Haiti

Wanajeshi 2 wa vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa wameuawa nchini Haiti.Wanajeshi hao,raia wa Jordan walikuwa wakipiga doria walipovamiwa na kundi la watu wenye silaha katika mtaa wa Puerto Principe wenye umasikini na hatari kubwa sana. Serikali ya Jordan imethibitisha vifo hivyo lakini imesema,haitojitoa kutoka ujumbe huo wa kulinda amani nchini Haiti.Vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa vina wajibu wa kurejesha usalama na utulivu katika kisiwa hicho cha Karibea.Tangu kupinduliwa kwa rais wa zamani Jean-Bertrand Aristide hapo mwaka 2004,wafuasi wake wanajaribu kuivuruga nchi hiyo kwa kufanya mashambulio mbali mbali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com