Polisi nchini Afghanistani wanawasaka wauaji wa waandishi wa habari wawili wa Deutsche Welle | Habari za Ulimwengu | DW | 10.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Polisi nchini Afghanistani wanawasaka wauaji wa waandishi wa habari wawili wa Deutsche Welle

Waziri wa mambo ya ndani wa Afgahanistani amesema kwamba hawajafanikiwa kuwakamata watu waliohusika na mauaji ya waandishi wa habari wawili wa Radio hii ya Deutsche Welle katika eneo hilo. Karen Fischer na Christian Struwe walipatikana wameuawa kwa kupigwa risasi katika mkoa wa Baghlan. Deutsche Welle ilisema waandishi hao wawili walikuwa wakifanya utafiti kwa shughuli zao za kibinafsi. Jana, wafanyakazi wa Radio Deutsche Welle mjini Bonn, waliomboleza kifo cha wenzao hao wawili. Mkurugenzi mkuu wa Deutsche Welle, Erik Bettermann, alisema kuwa Deutsche Welle itaendelea kusaidia katika ukarabati wa Afghanistani katika kuwatendea haki wafanyakazi hao waliouawa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com