1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Deutsche Bahn

Deutsche Bahn AG ni shirika la usafiri wa reli la Ujerumani. Likiwa na makao yake makuu mjini Berlin, shirika hilo ni la ubia la kibinafsi, ambapo shirikisho la Ujerumani ndiye mwanahisa pekee.

Deutsche Bahn inajinasibu kuwa shirika la pili kwa ukubwa la usafirishaji duniani baada ya shirika la Posta na usafirishaji la Ujerumani – Deutsche Post/DHL, na ndiyo shirika kubwa zaidi la umiliki na uendeshaji wa miundombinu ya reli barani Ulaya. Linabeba karibu abiria bilioni mbili kila mwaka. Katika ukurasa huu utapata maudhui za DW kuhusu Deutsche Bahn.