Osama bin Laden atoa ukanda mpya wa video | Habari za Ulimwengu | DW | 30.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Osama bin Laden atoa ukanda mpya wa video

Kiongozi wa kundi la al Qaeda, Osama bin Laden, ametoa ukanda mpya wa video. Katika ujumbe wake kwenye ukanda huo kiongozi huyo ametoa onyo kali dhidi ya Israel, akisema anapanga kupanua vita vya jihad katika eneo hilo ili kuikomboa ardhi ya Palestina.

Osama bin Laden pia ameishutumu Marekani kwa kutaka kuitawala Irak na amewaonya waislamu wa madhehebu ya sunni nchini Irak dhidi ya kujiunga na mabaraza ya kimbari kupambana na al qaeda au kushiriki kwa njia yoyote katika serikali ya umoja wa taifa.

Jana waziri wa mambo ya ndani wa Irak alitangaza kwamba asilimia 75 ya mtandao wa al qaeda umeharibiwa nchini Irak.

Jeshi la Marekani pia limetangaza kwamba linavishinda vita dhidi ya al qaeda nchini Irak, lakini likaongeza kwamba kundi hilo bado litakuwa changamoto kubwa katika mwaka ujao.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com