1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Mohammad Bin Salman Al Saud

Mohammad bin Salman bin Abdulaziz Al Saud, maarufu kwa kifupi kama MbS ndiye mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia.

Jina la ke kamili ni: Mohammad bin Salman bin Abdulaziz bin Abdul Rahman bin Faisal bin Turki bin Abdullah bin Mohammed bin Saud. Ndiye naibu waziri mkuu wa sasa (nafasi ya waziri mkuu inashikiliwa na Mfalme),na pia ndiye mwenyekiti wa Baraza la Maendeleo ya Kiuchumi, mwenyekiti wa baraza la masuala ya usalama na siasa, na waziri wa ulinzi. Ameelezwa kuwa ndiye nguvu nyuma ya kiti cha ufalme wa baba yake, mfalme Salman. Aliteuliwa kuwa mrithi wa kiti cha ufalme Juni 2017, kufuatia uamuzi wa Mfalme Salma kumuondoa Muhammad bin Nayef kutoka nafasi zake zote, na kumfanya Muhammad kuwa mrithi mteule wa kiti cha ufalme.

Onesha makala zaidi