Nusu-finali kombe la ulaya | Michezo | DW | 23.06.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Nusu-finali kombe la ulaya

Ujerumani ina miadi kesho na uturuki kabla Spian kucheza na Russia.

Baada ya mapumziko ya jana na leo, kombe la Ulaya la mataifa, linarudi uwanjani kesho kwa nusu finali ya kwanza:

Mabingwa mara 3 wa Ulaya na dunia-Ujerumani, wana miadi kesho na Uturuki.Siku ya pili yake alhamisi, itakua zamu ya -Spian na Russia.

Timu gani 2 zitacheza finali jumapili ijayo,itajulikana baada ya firimbi ya mwisho hapo alhamisi.

►◄

Kombe la Ulaya laimeingia hatua ya nusu-finali kesho na keshokutwa.

Mabingwa mara 3 wa Ulaya Ujerumani wana miadi kesho na Uturuki.Baada ya duru ya robo-finali kuzipiga kumbo nje ya mashindano washindi 3 wa makundi-Croatia,Holland na Urenoi,Ujerumani sasa inapigiwa upatu ndio itakayoibuka mabingwa jumapili ijayo.Kwanza lakini, inapaswa kutamba kesho mjini Basel,Uswisi dhidi ya Uturuki.

Baada ya kupepesuka katika duruya kwanza ilipozabwa mabao 2:1,Ujerumani ilifufuka baada ya kuwatoa wenyeji Austria,mjini Vienna, kwa bao 1:0.Halafu mizinga ya Ujerumani ikaelekezwa kwa wareno.

Manuwari ya wareno ikazamishwa kwa mabao 3-2-shukurani kwa mchezo maridadi wa chipukizi Bastian Schweinsteiger na nahodha,Michael Ballack lakini pia Lukas Podolski.

Ikiwa Ujerumani itaendeleza mchezo wsake huu,itakua vigumu kwa waturuki kesho kufua dafu.Lakini, wajerumani wamejifunza kuwa kama wao,waturuki hawakati roho na mapema na wanapigana kidume hadi firimbi ya mwisho kulia.

Mlinzi wa Ujerumani -maarufu kwa hujuma zake kutoka nyuma hadi lango la adui-Philip Lahm anasema mpambano wa kesho utakua mgumu,lakini ana matumaini Ujerumani itafua dafu:

Kipa wa Ujerumani -zamani Arsenal London, Jens Lehamann, anadai ni uzuri kukutana na Uturuki mara hii.Binafsi amekulia na wsaturuki katika mkoa wa Ruhr,amecheza nao dimba na anawapenda.

Ikiwa Uturuki watalifumania lango lake kesho na kutia bao, pengine Lehmann atayadurusu mapenzi yake kwa waturuki.

Spian, walivunja mwiko wa miaka 88 hapo jumapili walipowazaba mabingwa wa dunia-itali mabao 4-2 kupitia mikwaju ya penalty.

Timu hizo 2 zilitoana jasho kwa muda wa dakika 120 na mwisho,Spain ikatambaa.Spian lakini yaweza mara hii kukumbana na shida mbele ya warusi walioipiga kumbo Holland kwa mabao 3:1 hapo jumamosi.

Ndio Spian, iliizaba Urusi mabao 4:1 katika duru ya kwanza, lakini alhamisi hii,Spian huenda ikakutana na timu tofauti kabisa na ile wasliocheza nayo mara ya kwanza.Spian, ina kiu kikubwa cha kutawazwa mabingwa wa Ulaya,kwani tangu walipolitwaa kombe mara pekee 1964 ni kitambo kirefu kimepita,.Kocha wa urusi mholanzi guus Hiddink,anaandaa mtego mwengine kama ule uliowanasa wadachi.

Spain mara hii itatumai mastadi wake 2 David Villa na Fernando Trorres waliozimwa na walinzi wa Itali majuzi, wataweza kutamba mbele ya ngome ya Urusi.Waspian wana kiu kikubwa.Warusi walicheza finali ya kombe hili na Holland, 1988.Wangependa kucheza tena jumapili hii,Juni 29 mjini Vienna.