NEW YORK: Al Zawahri ataka serikali fisadi za kiislamu zipinduliwe | Habari za Ulimwengu | DW | 05.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Al Zawahri ataka serikali fisadi za kiislamu zipinduliwe

Naibu kiongozi wa kundi la kigaidila al Qaeda Ayman al Zawahri ameonekana kwenye ukanda mpya wa video katika tovuti inayotumiwa na makundi ya wanamgambo wa kiislamu, akitoa mwito kuwe na umoja katika vita vitakatifu vya jihad.

Kiongozi huyo pia ametaka serikali fisadi za kiislamu zipinduliwe. Kwenye ukanda huo al Zawahri alieleza kwa kina ufisadi wa familia ya kifalme ya Saudi Arabia na kulaani vikali hatua ya Palestina kukubali matakwa ya Israel.

Kiongozi huyo pia aliikosoa serikali ya Misri akiitaja kuwa mshirika wa Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com