NAIROBI : Wahukumiwa kifo kwa kumshambulia wa Thiongo | Habari za Ulimwengu | DW | 15.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI : Wahukumiwa kifo kwa kumshambulia wa Thiongo

Mahkama ya Kenya leo hii imewahukumu adhabu ya kifo walinzi watatu wa usalama kwa kumshambulia na kumpora mwandishi mashuhuri wa riwaya nchini humo Ngungi wa Thiongo.

Wakati wa kurudi nyumbani baada ya kuwa uhamishoni kwa hiari yake mwenyewe Thiongo alipigwa vibaya sana na watu wanne kwenye nyumba yake mjini Nairobi.Mke wake Njeeri alibakwa na kuunguzwa kwa moto wa sigara wakati wa usiku wa tukio hilo hapo mwezi wa Augusti mwaka 2004.

Wakati akitowa hukumu huyo Hakimu Mkuu Julie Oseko amesema kosa la wizi wa kutumia nguvu limekuwa likivuma jijini Nairobi na lazima lipigwe vita kwa kutowa adhabu kali.

Washtakiwa hao watatu Richard Kayago Maeta,Elias Sikukuu Wanjala na Peter Mulati Wafula walipatikana na hatia hapo Jumaatano na wamesema watakata rufaa.

Wakati hukumu ya kifo inaendelea kubakia katika sheria za Kenya haikutumiwa tokea wahusika wa kufanya mapinduzi miaka ya 1980 kunyongwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com