NAIROBI: Kibaki kuitisha mkutano wa IGAD kuijaidili Somalia
1 Januari 2007Matangazo
Rais Mwai kibaki wa Kenya amewataka viongozi nchini humo wakome kuwachochea wananchi huku uchaguzi mkuu ukitarajiwa kufanyika mwaka huu nchini humo. Huku kampeni za uchaguzi zikikaribia kuanza rais Kibaki amewataka viongozi washirikiane kudumisha umoja wa kitaifa.
Aidha rais Kibaki amesema kama mwenyekiti wa IGAD ataitisha mkutano wa kilele wa muungano huo hivi karibuni ili kuijadili hali nchini Somalia.