NAIROBI: Andre achaguliwa mjumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Somalia
19 Juni 2007Matangazo
Umoja wa Ulaya umemteu mjumbe wake maalum nchini Somalia,kusaidia juhudi za kuleta hali ya utulivu katika taifa hilo lililovurugwa kwa vita.Mjumbe huyo ni Georges-Marc Andre aliewahi kuwa msimamizi wa shughuli za umoja huo,nchini Gambia na Burundi.Bw.Andre ambae ni Mbeligiji,atakuwa na makao yake katika mji mkuu wa Kenya,Nairobi.