Nüremberg watwaa kombe la DFB | Michezo | DW | 28.05.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Nüremberg watwaa kombe la DFB

Nüremberg wamewazima mabingwa Stuttgart kutoondoka na vikombe vyote 2 -kombe la Ligi na kombe la shirikisho nyumbani.Waliwalaza stuttgart kwa mabao 3-2 baada ya kurefushwa mchezo jumamosi.

Nüremberg yatawazwa mabingwa wa kombe la DFB

Nüremberg yatawazwa mabingwa wa kombe la DFB

Ni Nüremberg na sio mabingwa Stuttgart waliotoroka jumamosi na Kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani-DFB Pokale-

Bafana Bafana –Afrika Kusini yaichapa Mauritius mabao 2:0 ili kukata tiketi ya nusu-finali ya Kombe la COSAFA.Nigeria yailaza Harambee Stars-kenya bao 1:0 mjini Nairobi huku Ugandan Cranes na Taifa Stars ya Tanzania zikijionoa kwa changamoto za jumamosi ijayo kuania tikieti za finali ya kombe la Afrika la mataifa 2008 nchini Ghana.Franz Beckenbauer,kuwa balozi wa FIFA kusaidia nchi masikini kukuza dimba.

Ni kitambo kirefu tangu mabingwa wa zamani wa ujerumani Nüremberg,kuvaa taji.jumamosi iliopita walikata nao kiu chao cha muda mrefu walipowatia munda mabingwa wapya wa Ujerumani VFB Stuttgart walipowachapa mabao 3-2 baada ya kurefushwa mchezo.Nüremberg ngoma yao ikivuma sana zamani na walitwaa ubingwa mara 9 kabla ya zama za Bayern Munich,FC Cologne,Hamburg au Borussia Mönchengladbach na Dortmund.

Kuanzia kombe la kwanza la ubingwa la Ujerumani 1920 hadi la mwisho 1968,Nüremberg ikitamba.

Nüremberg imerudi jumamosi kileleni mwa dimba la ujerumani –kwani ni timu pekee iliothubutui msimu huu kuilaza Stuttgart mara 3-mbili katika Ligi na 1 katika kombe la shirikisho la Ujerumani.Hivyo,imeinyima Stuttgart nafasi ya kutwaa vikombe vyote 2-Ligi na kombe la taifa.

Kocha wa Nüremberg, mjerumani mashariki Hans Meyer baada ya ushindi huo aliahidi makubwa zaidi yatafuata.Alisema,

“Tazarajia katika siku chache zijazo tutakuwa na shangwe kubwa zaidi.”

Nae meneja wa Nüremberg alielezea hivi ushindi wa timu yake hapo jumamosi:

“Ni wazi kabisa tumeishinda Stuttgart mara 3 msimu huu nah ii labda ilitupa nafuu kiakili kuliko Stuttgart.”

Stuttgart iliuonaje mpambano wa jumamosi:

Shabiki wao mmoja alisema:

“Nasikitika kuwa tumeshindwa ,nadhani yatupasa kuipongeza Nüremberg kwa ushindi wake.Kwani, wametushinda mara 3 msimu huu na kwahivyo wamestahiki kuwa mabingwa wa DFB Pokale.”

Nje ya kombe la Shirikisho la dimba la Ujerumani,FIFA-shirikisho la kabumbu ulimwenguni,limetangaza kuwa kuanzia sasa ni marufuku kuchezwa mechi za kitaifa katika viwanja viliopo mita zaidi ya 2.500 kutoka upeo wa bahari.Bolivia imeandaa mashindano ya kombe la dunia katika uwanja wake uliopo mita 3,600 kutoka upeo wa bahari.hii yaonekana na FIFA inaleta dhara kwa wachezaji dimba.

Franz Beckenbauer wa Ujerumani, atakalia kiti alhamisi hii ijayo cha katika kamati-tendaji ya FIFA.Beckenbauer amesema, angependa kuwa balozi wa FIFA kusaidia nchi masikini kabisa zanachama wa FIFA.Akasema, Afrika Kusini inapaswa kusaidia kikamilifu ili kufaulu kuandaa kombe la dunia 2010.

Jumamosi ijayo itakua “asie na mwana aeleke jiwe “barani Afrika:timu kadhaa za taifa zitakuwa uwanjani kukata tiketi zao za finali ya mwakani ya kombe la Afrika la mataifa.

Tanzania ina miadi na Senegal,Kenya na Swaziland na Uganda na Nigeria:Nigeria ikiongozwa na kocha wa taifa wa zamani wa Ujerumani Berti vogts ilijipima nguvu mjini Nairobi na Harambee Stars:Nigeria iliitoa Kenya kwa bao 1:0 kabla kuvuka mpaka kwenda Kampala kwa miadi na Ugandan cranes Juni 2.

Na mjini Dar-es-salaam,Taifa Stars iliopimana nguvu na Uganda hivi majuzi inapania kwa changamoto nyengine na Senegal.Safari hii wakicheza nyumbani,Taifa Stars watakua na mchezaji 1 zaidi-rais wao Jakaya Kiwete atakuwa uwanjani.

Katika kinyan’ganyiro cha kombe la COSAFA-kombe la shirikisho la dimba la kusini mwa Afrika.

Bafana Bafana- timu ya Afrika Kusini jana iliizaba Mauritius mabao 2:0 huko Swaziland na kukata tiketi yake ya nusu-finali.Teko Modise,ndie alieufumania mlango wa Mauritius mara zote 2 na kukaribishwa ndani.Kocha wa Bafana Bafana-mbrazil Carlos Alberto Parreira aliwateremsha wachezaji 4 wapya.

Swaziland nayo ikailaza Malawi bao 1:0.Afrika Kusini, sasa inajiunga na Msumbiji na Zambia pamoja na Angola katika nusu-finali ya kombe la castle cup huko Botswana hapo Julai.

 • Tarehe 28.05.2007
 • Mwandishi Ramadhan ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHc9
 • Tarehe 28.05.2007
 • Mwandishi Ramadhan ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHc9