Mwandishi wa habari mfaransa kushtakiwa kwa kusafiri bila kibali | Habari za Ulimwengu | DW | 22.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mwandishi wa habari mfaransa kushtakiwa kwa kusafiri bila kibali

Naibu waziri wa usalama wa eneo la Puntland, Farah Abdi Dolshe, amesema leo kwamba huenda wakamfungulia mashtaka mwandishi wa habari raia wa Ufaransa kwa kukiuka sheria za uhamiaji wakati atakapoachiliwa.

Bwana Dolshe amesema mpigaji picha wa kifaransa, Gwen Le Gouil, ambaye anazuiliwa na watekaji nyara, alikuwa akisafiri bila kibali.

Kiongozi huyo ameongeza kusema mazungumzo yanaendelea kati ya utawala wa Puntland, maafisa wa Ufaransa na watekaji nyara kujaribu kumuokoa mwandishi huyo wa habari licha wa watekaji nyara kudai walipwe dola 80,000 kabla kumuachilia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com