1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanajeshi wa Denmark auwawa Afghanistan.

27 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DVeS

Kabul.

Mwanajeshi mmoja wa Denmark ameuwawa na mwingine amejeruhiwa katika mapambano ya silaha na wapiganaji wa Taliban kusini mwa Afghanistan.

Jeshi la kimataifa la usaidizi wa usalama limesema leo kuwa raia hao wa Denmark walikuwa katika doria katika jimbo la Helmand wakati waliposhambuliwa. Denmark imepoteza hadi sasa wanajeshi 13 nchini Afghanistan. Wadenmark wengine wawili waliuwawa March 17 katika shambulio dhidi ya msafara wa wanajeshi wa jeshi hilo la NATO. Zaidi ya wanajeshi 30 wa jeshi hilo la kimataifa wameuwawa nchini Afghanistan mwaka huu.