Muimlas wa zamani wa Chile Pinochet afunguliwe mashtaka | Habari za Ulimwengu | DW | 28.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Muimlas wa zamani wa Chile Pinochet afunguliwe mashtaka

SANTIAGO:

Muimla wa zamani wa Chile AUGUSTO PINOCHET anakabiliwa na kesi nyengine mahakamani.Jaji mmoja nchini Chile amemshitaki Pinochet kuhusika na mauwaji , mateso pamoja na kutoweka watu kadhaa kaati ya mwaka 1974 na 1977 katika jela ya Villa Grimaldi nchini Chile.Takwimu rasmi zinazungumzia juu ya watu 220 waliouwawa katika jela hiyo.Muimla huyo mwenye umnri wa miaka 90 amekanusha madai yote dhidi yake.Juhudi zote za kutaka kumfikisha mahakamani Augusto Pinochet zimekua zikishindwa hadi wakati huu kwasababu ya afya yake dhaifu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com