Mugabe awasili Ureno tayari kwa mkutano wa EU-AU | Habari za Ulimwengu | DW | 07.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mugabe awasili Ureno tayari kwa mkutano wa EU-AU

LISBON.Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewasili mjini Lisbon Ureno tayari kwa mkutano wa wakuu wa Afrika na Ulaya utakaoanza kesho.

Rais Mugabe ambaye kuhudhuria kwake mkutano huo, kumemfanya Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown kususia aliwasili mjini Lisbon jana saa mbili usiku na moja kwa moja na msafara wake alielekea hoteli.

Ingawa Umoja wa Ulaya umemuwekea vikwazo vya kusafiri, kwa tuhuma za kuuvuruga uchaguzi wa mwaka 2002 ambapo alichaguliwa tena, Mugabe alipewa mualiko wa kuhudhuria baada ya viongozi wenzake wa Afrika kutishia kususia mkutano huo iwapo asingealikwa.

Wakati huo huo wabunge wa nchi za Ulaya na Afrika wanaokutana mjini Lisbon kabla ya mkutano huo wa kilele wamewataka wakuu hao kulitupia macho suala la Darfur.

Wamesema kuwa iwapo wakuu hao watashindwa kushughulikia mzozo huo wa Darfur basi itakuwa ni kuyapa kisogo masahibu yanayowakuta watu wa Darfur.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo mwezi Julai liliidhinisha kupelekwa kwa kikosi cha askari jeshi na polisi elfu 26 wa umoja huo na ule wa Afrika kulinda amani katika jimbo hilo lenye mzozo la Darfur.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com