1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Kudi la waasi wa Chechnya lasakwa Waziri wa ulinzi wa Russia ...

17 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFrb

Sergei Ivanov ameviamuru vikosi vya nchi yake kulikamata likiwa hai au hata kuliuwa kundi la waasi wa Chechnya lililouhusika na mauaji ya wanajeshi tisa wa mpakani wa Russia. Madarzeni ya wapiganaji wa chini kwa chini waliwauwa walinzi hao wa mpakani mapema siku ya Jumamatu katika kile kinachonekana kuwa shambulio la wazi kwenye mpaka wa milimani na Jamhuri ya kusini mwa Russia ya Dagestan.Takriban watu 12 walitekwa na kushikiliwa mateka lakini ilipofika usiku mateka hao waliachiliwa huru na wapiganaji hao wa chini kwa chini kukimbilia milimani.Afisa wa mmoja wa serikali amesema wapiganaji hao Wachechen hakutowa vitisho kwa mateka wao wala madai yoyote yale ya kisiasa. Kufuatia tukio hilo hali ya hatari imetangazwa huko Dagestan.