1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Chechnya

Jamhuri ya Chechen, au Chechnya, ni jamhuri ya Urusi, inayokutikana katika eneo la Caucasus Kaskazini, kusini kabisaa mwa Ulaya Mashariki, na siyo mbali na Bahari ya Caspian. Mji Mkuu wa Chechnya ni Grozny.

Baada ya kuvunjika kwa muungano wa Kisoviet mwaka 1991, eneo hilo liligawiwa katika sehemu mbili: Jamhuri ya Ingushetia na Jamhuri ya Chechen, ambayo ilitaka uhuru wake. Kufuatia vita ya Chechnya na Urusi, Chechnya ilipata kile kinachofanana na uhuru, lakini udhibiti wa shirikisho la Urusi ulirejeshwa baada ya vita vya vipili vya Chechnya. Mapigano ya hapa na pale yanaendelea katika milima na mikoa ya kusini ya jamhuri hiyo. Ukurasa huu ni mkusanyiko wa maudhui za DW kuhusu jamhuri ya Chechnya.