MOSCOW: Urusi yalikataa ombi la Uingeraza | Habari za Ulimwengu | DW | 05.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW: Urusi yalikataa ombi la Uingeraza

Urusi imepuuza rasmi ombi la Uingereza la kuitaka nchi hiyo impeleke mshukiwa mkuu katika mauaji ya kachero wa zamani wa Urusi aliyeuwawa nchini Uingereza Alexander Litvinenko.

Kwa mujibu wa afisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Uingereza, Urusi ilitamka kupitia kwa waandishi wa habari kwamba haitamtoa mshukiwa huyo mkuu Andrei Lugovoy lakini wakati wote huo Uingereza ilikuwa inasubiri mawasiliano rasmi kutoka kwa serikali ya Urusi.

Afisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Urusi imeifahamaisha wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza kwamba ni kinyume cha sheria kuambatana na kifungu nambari 61 cha sheria za Urusi kumtoa raia wa nchi hiyo kwenda kushtakiwa katika nchi ya kigeni.

Kesi hiyo imezusha mvutano wa kidplomasia kati ya Moskow na London.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com