1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Crimea

Crimea ni rasi iliyoko katika pwani ya kaskazini ya Bahari Nyeusi. Baada ya kuanguka kwa Jamhuri ya Muungano wa Kisovieti mwaka 1991, Crimea ilikuwa sehemu ya nchi huru ya Ukraine, na hivyo kusababisha mzozo na Urusi.

Mwaka 1954, Crimea ilihamishiwa kwa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Kisovieti ya Ukraine kama hatua ya kiishara na kiongozi wa Muungano wa Kisovieti Nikita Khrushev. Baada ya kuvunjika kwa muungano wa Kisovieti mwaka 1991, Crimea iliachwa kuwa sehemu ya Ukraine huru. Meli za kivita za Urusi katika Bahari Nyeusi zimewekwa katika kisiwa cha Sevastopol na ncha ya kusini ya rasi hiyo inaendelea kuwa ngome ya Urusi katika kanda. Katika miongo iliyopita, mzozo umekuwa ukifukuta baina ya majirani hao wawili, lakini haukufikia kiwango cha kupeleka majeshi cha Machi 2014. Tangu wakati huo, eneo hilo liko chini ya udhibiti wa Urusi. Ripoti za karibuni za DW kuhusu Crimea zinapatikana hapa.

Onesha makala zaidi