MOGADISHU : Watu 9 wauwawa katika shambulio la roketi | Habari za Ulimwengu | DW | 09.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU : Watu 9 wauwawa katika shambulio la roketi

Takriban Wasomali 9 wameuwawa na wengine madarzeni kujeruhiwa hapo jana wakati roketi lililofyetuliwa kwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika kupiga mkahawa katika shambulio ambalo pia limewajeruhi kidogo wanajeshi wawili wa kulinda amani.

Shambulio hilo la jana ni la pili dhidi ya wanajeshi wa Uganda ambao ni kikosi tangulizi cha Umoja wa Afrika na ambao wamekuwa shabaha ya mashambulizi mara tu baada ya kuwasili hapo Jumanne.

Waasi wamekuwa wakifanya mashambulizi takriban kila siku dhidi ya serikali ya mpito na washirika wake Ethiopia katika kipindi che miezi miwili iliopita na pia wametishia kukishambulia kikosi cha Umoja wa Afrika.

Kombora lililovurumishwa na roketi lilokusudia kushambulia gari la deraya la Umoja wa Afrika imelikosa gari hilo na badala yake limeripuwa mkahawa na kujeruhi watu 26 wakiwemo wanawake na watoto.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com