Mkutano wa UM Doha | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.12.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mkutano wa UM Doha

Mkutano wa miradi ya maendeleo kwa nchi changa huko Doha umemalizika.

Jana jioni ulimalizika mjini Doha, mji mkuu wa Gatar,mkutano wa Umoja wa Mataifa wenye shabaha ya kuhakikisha miradi ya maendeleo ilivyoafikiwa katika kikao cha 2002 cha Monterrey,nchini Mexico inatekelezwa. Mada mfano raslimali za kigeni,kupunguza madeni na mifumo bora ya ulipaji kodi , ilijadiliwa kama pia kiwango cha juu cha misaada ya maendeleo. Mkutano huu lakini, uligubikwa na wingu la msukosuko wa sasa wa fedha ulimwenguni.Ili kujadili athari zake kwa nchi changa,wajumbe waliafikiana huko Doha,kuitisha kikao kingine zaidi pengine hapo mwakani.

Ilikua rahisi kuufanyia mzaha mkutano huu wa Doha, jinsi ulivyozungumzia namna ya kugharimia misaada ya maendeleo .

Uliandaliwa kwa mwaka mzima .Halafu wajumbe 192 wakafunga safari kutoka kila pembe ya dunia ili kukutana na waakilishi wa mashirika yasio ya kiserikali na vyombo vya habari katika hoteli la kifahari mjini Doha,Gatar.Baada ya kupita siku 4 za majadiliano marefu ,waliafikiana kile kile ambacho miaka 7 iliopita mkutano uliafiki kuwa si kibaya,lakini chaweza kuendelezwa.Ili kukiendeleza, mkutano umepanga mkutano mwengine mwakani.

Kama tulivyosema haikuwa taabu kuufanyika dhihaka mkutano huu wa Doha na kusema si chochote wala si lolote isipokuwa lilikuwa porojo tupu.Ni porojo ambalo hata wanasiasa mashuhuri hawakuhudhuria.

Lakini mada iliozungumwsa ilistahiki kuzungumzwa.Lakini barabara na kwa nia safi.Kwani, azma yake ni kupiga vita umasikini,njaa na ufukara ulimwenguni na kujaribu kuwewezesha binadamu wengi kama iwezekanavyo kuishi maisha bora. Ni kikao kilichowakilisha mila na tamaduni mbali mbali na hata mifumo tofauti ya kisiasa tena kutoka nchi 192 zanachama wa UM.

Tusijaribu kwahivyo kuona mambo ni rahisi hivyo.

Hebu tufikirie ,kikao hiki hakikuzungumzia hali ya uchumi na shida zake zote,bali ni kujenga maskani njema kwa sote.Matajiri wamezowea kuona majumba yao hayadhurwi na hali yoyote ya hewa.mvua jua .Masikini lakini katika vibanda vya makuti na mbao hawana hata nyumba kama hizo za kuvumilia hali ya hewa .Kwsahivyo shabaha iliowekwa na wote ni kuwapatia wote maskani bora.

Nchi tajiri zilitangaza zitayari kuchangia sehemu ya nyumba hizo kwa masikini,kiasi kidogo.Kwani, hata nazo zina misukosuko yao wakati huu.

Kwahivyo, wote wakajumuika pamoja -matajiri na maskini ili kuafikiana vipimo vya nchini kabisa ya kuwapatia wote maskani mema .Wakaafikiana kuwa nyumba bora iwe na kuta 4 na paa.Wakaafikiana kujenga nyumba ambazo ukija upepo wa kwanza hazitaporomoka.

Shabaha hizo lakini ,hata hazikufikiwa huko Doha,kwani wakati huu wanazungumzia alao kuwa na nyumba imara za kujishikiza.Walikutana kujua juhudi hizo zimefikia wapi na kuamua kipi zaidi kifanywe.

Halafu ghafula na kwa msangao wa wengi,ukaibuka ufa nakusema wazi -mpasuko katika nyumba za mawe ,kwani mmoja kachanganya mchanga mwingi na seruji.Mafundi-mainjinia wa dola tajiri hawakugundua kosa hilo.

Wakati majumba ya matajiri yanayumbayumba ,wanazungumza sasa juu ya vibanda vya makuti vya masikini.Wakaafikiana tu kwamba siku zijazo wajenge nyumba ambazo alao ukipiga upepo wa kwanza zisiwe kama zile za karata zinaanguka.Nchi tajiri zikaahidi tena kuzisaidia nchi masikini katika shabaha hiyo.asikini lakini sasa wameingiwa na shaka shaka na danganyatoto hiyo.wanadai sasa mazungum,zo wazi ya kuchanganya seruji hasa na mchanga. Alao kuf

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com