Mkutano wa OSCE . | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 02.12.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mkutano wa OSCE .

Mkutano wa OSCE kukamilika hii leo.

default

Rais wa Kazakhstan Nursultan Nazarbayev, na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

Viongozi wa dunia wametoa wito wa pamoja wa kuwepo shirika lenye nguvu la usalama na ushirikiano Ulaya, OSCE, katika mkutano wa kwanza wa shirika hilo tangu mwaka 1999 nchini Kazakhstan.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel  amesema shirika hilo lenye wanachama 56 lazima kwanza lihakikishe amani na uhuru inakuwepo katika mipaka yake. Akiigusia  nchi mwenyeji, Merkel amesema hakikisho la haki za binaadamu na uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya habari, ni lazima utekelezwe.

OSZE Gipfel in Kasachstan NO FLASH

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Rodham Clinton,na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel katika mkutano wa OSCE.

 Kazakhstan ni nchi ya kwanza ya iliyokuwa muungano wa Sovieti  kushikilia uwenyekiti wa shirika hilo. Waandishi wa habari wasio na mipaka wamesema nchi hiyo haifai kuandaa mkutano huo kwani haifikii viwango vya shirika hilo.

OSCE liliundwa wakati wa vita baridi kama njia ya majadiliano kati ya mataifa ya kikomyunisti na Magharibi.

Mwandishi Maryam Abdalla/DPAE

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com