Mkutano wa NATO | Matukio ya Kisiasa | DW | 07.03.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mkutano wa NATO

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za mfungamano wa kijeshi wa NATO wameshindwa kufikia mapatano juu ya kuupanuza mfungamano wao.

default

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za NATOMawaziri wa mambo ya nje wa nchi za mfungamano wa kijeshi -NATO wameshindwa kuafikiana juu ya kuwaingiza wanachama wapya katika mfungamano wao lakini viongozi wa nchi hizo watakutana tena mwezi ujao mjini Bukarest.

Utata ulitokea kwenye mkutano huo kutokana  na Ugiriki kupinga Mecccedonia kuingizwa katika mfungamano huo kutokana  na nchi mbili hizo kuzozana  juu ya jina hilo Maccedonia. Ugiriki inasema kwa Maccedonia kutumia jina hilo maana yake ni kutoa madai juu ya sehemu yake ya kaskazini yenye jina kama hilo.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za mfungamano wa kujihami-NATO kwenye mkutano wao pia walijadili uanachama wa Albania na Croatia.

Ugiriki imesema haina kipingamizi juu ya nchi hizo mbili. Lakini ilitishia kutumia kura ya veto kuzuia Maccedonia kupewa uanachama wa NATO.

Mawaziri wa NATO, pia walitafakari uwezekano wa Ukraine na Georgia kuingizwa katika uanachama wa mfungamano wao.

Lakini Ujerumani na Ufaransa zimeeleza mashaka juu ya hayo. Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa bwana Kouchner amewaambia wandishi habari kuwa nchi yake inazingatia kuwa ni jambo muhimu sana kwa Umoja wa Ulaya kuendeleza uhusiano mzuri na Urusi.

Hatahivyo  katibu mkuu wa NATO Jaap

de Hoop Scheffer amesisitiza umuhimu wa NATO katika kudumisha amani barani Ulaya.

Viongozi wa nchi na serikali wa madola ya Nato wanatarajiwa kukutana mjini Bukarest Rumania  mwezi aprili ambapo masuala hayo yatatazamiwa kujadiliwa. 
 • Tarehe 07.03.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DKWV
 • Tarehe 07.03.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DKWV
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com