Mkutano wa kilele wa EU.
28 Oktoba 2010Matangazo
Mkutano huo unafanyika wakati, Ujerumani na Ufaransa zinakabiliwa na upinzani mkali kwa kutaka kwao mabadiliko katika mkataba wa Lisbon wa umoja huo.
Jana, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alitetea pendekezo la kutaka kuwepo kwa adhabu kali dhidi ya mataifa ya sarafu ya Euro yatakayoshindwa kufikia viwango vya mkataba wa Umoja wa Ulaya katika uthibiti wa uchumi.
Kansela Merkel anajiandaa kufanyia marekebisho mkataba wa sasa wa Lisbon kwa ajili ya kuweza kukabiliana na matatizo yatakayotokea baadaye kuhusiana na madeni.