Mkutano wa kilele wa Bologna | Matukio ya Kisiasa | DW | 12.03.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mkutano wa kilele wa Bologna

Mawaziri wa elimu wa Umoja wa Ulaya wazungumzia mageuzi.

Annette Schavan -waziri wa elimu.

Annette Schavan -waziri wa elimu.

Katika nchi nyingi za Umoja wa Ulaya, utaratuibu wa mageuzi ya vyuo vikuu unakosolewa mno. Mawaziri wa elimu wa nchi hizo, kwa hivyo,wamezikabili ila zilizotolewa katika mkutabno wao wa kilele huko Bologgna, nchini Italy.

Kimsingi, kikao hiki kilikuwa kiwe kama sherehe kubwa: kwani mwaka huu wa 2010, kwa muujibu wa mpango wa awali, ulilengwa kukamilisha mradi wa kuvifanyia mageuzi vyuo vikuu vya Ulaya. Lakini, miaka 10 kamili tangu kuanzishwa mageuzi hayo ,ilipangwa kuukamilisha utaratibu wa mageuzi wa Bolognia tena kwa mafanikio. Hivyo ndivyo ilivyopangwa mwishoni mwa 1990.Hivi sasa, lakini, hali imebainika hivi: Itachukua alao miaka 10 mengine ili kukamilisha mageuzi ambayo yaliamuliwa kufanywa huko Bologna,Italy. Kwa sura hii, sherehe za miaka kumi mjini Bolognia zilipungua kasi na kuwa ndogo kuliko ilivyopangwa kabla, na ikawa wakati wa kupitisha fikra nini kimeenda kombo.Bibi Sigrid Mauerer,mwenyekiti wa Jumuiya ya vyuo vikuu nchini Austria, anasema,

"Sisi tunaosoma vyuo vikuu, tunatarajia kuwa mawaziri wa elimu watambue wamechafua mambo mengi."

Akaongeza kusema zaidi kwamba, mradi wa Bolognia ni zaidi kuliko kujumuisha masomo ya shahada ya "ubachelor, Master na ya udaktari " pamoja. Hasa, alisema, maswali ya kijamii na swali la uwezo wa kujifunza hadi sasa hayakutiliwa maanani sawa sawa. Na hayo, ndio maswali ambayo sasa yanapaswa kujadiliwa na kurekebishwa-alidai.

Sawa kama ilivyokuwa miezi iliopita, mawaziri hao wa elimu wamekuwa wakisikia ila za wanafunzi na mara hii, hali haikuwa vyengine kama ilivyokuwa mjini Budapest (Hungary) na Vienna (Austria). Pongezi nyingi zilitolewa kwa wanafunzi chipukizi .Taarifa ya kuvutia iliosikika ni ile iliotolewa na na Umoja wa Wanafunzi, alisema waziri wa elimu wa Ujerumani, bibi Annette Schavan, siku ya kwanza ya mkutano wa Bologna.

Waziri huyo wa elimu wa Ujerumani, kwa ushirikiano na wanafunzi, anapanga kuurekebisha barabara utaratibu wa mageuzi yanayohitajika.Akawataka mawaziri wenzake wa elimu wa Ulaya, kwa jicho la matatizo ya mageuzi , kufanya kazi kwa bidii zaidi badala ya kusherehekea tu.

Bibi Schavan alisema zaidi kwamba, licha ya shida ziliopo, hakuna njia nyengine, isipokuwa kusonga mbele na mageuzi. Kati ya mwezi Mei , mwaka huu, waziri huyo wa elimu wa Ujerumani, akiitikia wimbi la malalamiko ya wanafunzi juu ya mageuzi ya vyuo vikuu mwishoni mwa mwaka jana , ameitisha kikao kingine cha Bologna mjini Berlin.

Kuwa hakuna sababu kubwa ya kusherehekea huko Bologna wakati huu, ndivyo pia, unaonavayo Umoja wa wa wanafunzi wa Ujerumani (DSW). Rais wake, Rolf Dobischat, anasemakuwa, itapasa kubakia kuyakosoa mageuzi hadi pale kote Ulaya, iwezekane kuchukua masomo ya shahada ya "Bachlor", na kuna wanafunzi ambao hawawezi kujifunza nchi nyengine za Umoja wa Ulaya na nafasi za kujipatia kazi kwa wanafunzi waliohitimu shahada za "Bachelor"bado ni duni na si wazi.

Mwandishi: Himmelrath,Armin

Mtayarishi: Ramadhan Ali/DW-Radio

Uhariri: Othman, Miraji

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com