Mkutano wa kilele :China na Umoja wa Ulaya | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 20.05.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mkutano wa kilele :China na Umoja wa Ulaya

China na UU zakutana leo mjini Prague-mada:biashara.

default

Wen Jiabao -waziri-mkuu wa China.

Leo unafanyika mkutano wa kilele kati ya China na Umoja wa Ulaya mjini Prague, Jamhuri ya Czech,mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya.

Biashara kati ya China na UU ingawa imeopngezeka mno,hatahivyo, kuna nafasi ya kuikuza zaidi.Pia biashara hiyo haiko katika mezani sawa-hivyo inahitaji marekebisho.Kwahivyo, kuna mada za kutosha leo mjini Prague .

Usuhuba kati ya China na Umoja wa Ulaya, sio kuwa hauna matatizo yake.La hasha.

Asili yake mkutano huu wa kilele mjini Prague, ulikuwa ufanyike Desemba mwaka jana ,lakini Beijing ikauvunja tena dakika ya mwisho.China ilikasirishwa na mkutano alioufanya mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya wakati ule Rais Nicholas Sarkozy wa Ufaransa na Dalai Lama,kiongozi wa watibeti.

Doris Fischer-bingwa wa m aswali ya China katika Taasisi ya ujerumani ya siasa za maendeleo anasema:

"Serikali ya China ilipaswa kuchukua msimamo juu ya mkutano huo na hata ikiwa kutokana na siasa za ndani ya Chiona .Lakini pia kwa muda mrefu ujao kisa kama hicho hakihatarishi uhusiano wa kibalozi."

Pale waziri mkuu wa China, Wen Jiabao na Kamishna wa Tume ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso pamoja na msemaji wa siasa za nje Javier Solana , wakikutana leo katika qasri la Praguie,bila shaka, watalikwepa sawali la Tibet ; na hii hata ikiwa Dalai Lama alidai mada hiyo izungumzwe.

Katika shina la mazungumzo ya leo mjini Prague kwa jicho la msukosuko wa kiuchumi ulimwenguni,mazungumzo yatatuwama zaidi katika sekta ya uchumi na biashara kati ya pande hizi mbili.

Kwani, biashara kati ya pande hizo mbili inaongezeka mno.Umoja wa Ulaya wakati huu ,ndie mshirika mkubwa na muhimu wa China. Kwa upande mwengine, China iko nafasi ya pili kwa bidhaa zinazosafirishwa na UU nchi za nje,Marekani ikishika nafasi ya kwanza. Na hapo ndipo tatizo kubwa lilipo katika biashara ya pande hizi mbili.

Mwaka jana ,Umoja wa Ulaya ulikuwa na biashara na China iliofikia Euro bilioni 320 na hii ni kasoro kwa upande wake ya kima cha Euro bilioni 170. Bibi Fischer asema:

"Kuwa kila kukicha , Umoja wa Ulaya unadai China ifungue zaidi masoko yake katika sekta fulani za bidhaa au China ,itimize ahadi ilizotoa katika shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO),wakati huo huo China nayo mara kwa mara, inabainisha wazi haitii maanani siasa ya Umoja wa Ulaya ya kupinga China kusheheni bidhaa zake katika masoko yao."

Mada zaidi zitazozungumzwa leo mjini Prague, ni ombi la China kuwa Umoja wa Ulaya, uiuzie zana za ufundi wa hali ya juu-(High-Tech).Na Umoja wa Ulaya, nao utadai China iheshimu zaidi hati-miliki za bidhaa za ufundi kama huo na kutoigizwa na China baadae.Karatasini,China imepiga hatua kubwa katika kutia nia ya kuheshimu haki hizo, kivitendo lakini bado iko mbali.

Mtayarishaji:Ramadhan Ali

Mhariri:M.Abdulrashman

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com