Mkutano wa kanda kutatuwa mzozo wa Sudan | Habari za Ulimwengu | DW | 20.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mkutano wa kanda kutatuwa mzozo wa Sudan

Viongozi wa kanda wanapanga kuwa na mkutano wa viongozi kutatuwa mgogoro unaokuwa nchini Sudan uliozushwa kutokana na kujiondowa kwa waasi wa zamani wa kusini mwa Sudan kutoka serikali ya umoja wa kitaifa.

Uamuzi huo umefikiwa katika mazungumzo tafauti nchini Kenya yenye kuwahusisha Rais Mwai Kibaki wa Kenya,Rais Yoweri Museveni wa Uganda ,Rais wa utawala wa ndani wa Sudan kusini Salva Kiir na Rais mstaafu wa Kenya Daniel arap Moi.

Moi mjumbe maalum wa amani wa Kenya kwa Sudan amekuwa na mazungumzo na Museveni hapo jana juu ya juhudi hizo ambapo Kenya ni mwenyekiti wa Mamlaka ya Kiserikali ya Maendeleo IGAD.

Kiongozi wa Sudan ya kusini Salva Kiir hapo jana ameishutumu serikali ya Sudan kwa kujiandaa kwa vita na waasi hao wa zamani wa kusini.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com