Mkutano kuhusu mgogoro wa Darfur
27 Oktoba 2007Matangazo
Lakini kuna shaka ikiwa mkutano huo utaweza kupata makubaliano ya maana,kwa sababu makundi makuu mawili ya waasi yamesusia mazungumzo hayo ya amani yanayosimamiwa na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.
Makundi hayo mawili ni Kundi la Haki na Usawa JEM na Umoja wa jeshi la Ukombozi wa Sudan SLA-Unity. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa,Jan Eliasson aliesaidia kutayarisha mkutano huo wa amani amesema,ni matumaini yake kuwa wataweza kuyashawishi makundi hayo mawili kuhudhuria mkutano huo.