Mkasa wa Marion Jones-malkia wa mbio fupi | Michezo | DW | 05.10.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Mkasa wa Marion Jones-malkia wa mbio fupi

Marion Jones anatazamiwa kufika mbele ya M;ahkama leo mjini New York na kuungama madhambi ya doping-matumizi ya madawa kuongeza kasi.

Marion Jones

Marion Jones

Katika mkasa mkubwa kabisa wa madhambi ya doping-matumizi ya madawa kuongeza kasi tangu kisa cha Mkanada Ben Johnson katika michezo ya Olimpik seoul, 1988, Marion Jones alietukuzwa “malkia wa mbio fupi”-mita 100,mita 200 na long jump- mwishoe nae,asemekana kwa muujibu wa WASHINGTON POST - ameungama kufanya madhambi hayo.

Je, atavuliwa mataji yake ya Olympic ya Sydney mwaka 2000 kama Ben Johnson kule Seoul ?

Ramadhan ali asimulia:

Marion Jones kwa muujibu wa gazeti hilo la Washington Post ameungama madhambi hayo katika barua aliowapelekea jamaa zake na marafiki.Anadai kocha wake alipa dawa iliodhihirika baadae ni ile inayokatazwa.

Marion Jones,kwa muda mrefu amekuwa akikanusha kutumia madawa kuongeza kasi,lakini tuhuma dhidi yake zilipambamoto baada ya kuhusishwa na maabara ya “BALCO LAB” ya San Francisco hapo 2004 iliotengeza dawa ya steroids maarufu kwa jina la THG au “The clear”.

Washington Post limeripoti katika mtandao wake kuwa mtu mmoja aliepata barua hiyo alimsomea ripota kwa njia ya simu.

Duru nyengine inayoelewa hali ya kisheria inayomkuta sasa Marion Jones akizungumza bila kutaka kutajwa ,alithibitisha yaliomo ndani ya barua hiyo.

Katika barua hiyo Marion Jones anaripotiwa kudai kuwa dawa hiyo “the clear” alipewa na kocha wake Trevor Graham aliemwambia ni aina ya mafuta yaliotengezwa kwa mbegu.

Marion Jones alifumaniwa na madhambi ya doping Juni 2006 kwa matumizi ya dawa iitwayo (EPO) lakini sampuli ya pili-B,ilimtakasa hana madhambi.

Novemba mwaka jana, kocha Graham alishtakiwa kwa kutoa taarifa za uwongo kwa wapelelezi wa polisi waliokuwa wakichunguza kisa hiki .Tangu wakati huo,orodha kubwa ya wanariadha chini ya kocha huyo wamegunduliwa kufanya madhambi:Na hapo august mwaka jana, wanariadha waliojifunza kwake walipigwa marufuku kuwa mwiko kushiriki katika finali ya mashindano ya riadha ya Golden League,mjini Berlin.

Rafiki wa kiume wa Marion Jones,bingwa wa zamani wa rekodi ya dunia Tim Montgomery,akabidi nae kupigwa marufuku miaka 2 kwa kugunduliwa kuhusika na maabara ya Balco Lab.

Mapema 2006,Marion Jones na muasisi wa maabara ya BALCO- Victor Conte, walifikia muafaka katika kesi ya madai ya dala milioni 25 aliotoa Marion Jones dhidi ya maabara hayo kwa kumharibia jina.Kwani, Jones alimshtaki Conte alipodai alimpa Jones dawa mbali mbali marufuku kabla na hata baada ya michezo ya 2000 ya olimpik ya Sydney.

Mkuu wa Kamati ya olimpik ya Australia John Coates amedai malkia huyu wa zamani wa mbio fupi apokonywe medali zake 3 za dhahabu na 2 za fedha alizoshinda katika michezo ya Sydney.

Taarifa zasema Marion Jones atafika leo mbele ya mahkama moja mjini NY na huko ataungama madhambi yake.

 • Tarehe 05.10.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/C7ne
 • Tarehe 05.10.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/C7ne
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com