Mkakati wa ushirikiano watiwa saini Lisbon
10 Desemba 2007Matangazo
Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika umemalizika Lisbon nchini Ureno kwa kutiwa saini mkakati mpya wa ushirikiano kati ya mabara hayo mawili.Viongozi wa pande mbili wameusifu mkakati huo kama ni matokeo ya kihistoria.Hata hivyo,mapendekezo ya Umoja wa Ulaya juu ya mkataba mpya wa biashara yamekataliwa na viongozi wengi wa Kiafrika.