Mji wa Haskanita wateketezwa moto | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 08.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mji wa Haskanita wateketezwa moto

Baada ya siku chache tangu askari 10 wa Umoja wa Afrika walipouwawa katika mji wa Haskanita kwenye jimbo la Darfur sasa wakaazi wake wamelazimika kuondoka kufuatia mji huo kuchomwa moto.

Rais Omar El Bashir wa Sudan

Rais Omar El Bashir wa Sudan

Umoja wa mataifa umearifu kwamba mji wa Haskanita iliko kambi ya kikosi cha kulinda amani cha umoja wa Afrika ambayo iliyovamiwa na waasi wiki iliyopita umevamiwa tena na kuchomwa moto.

Wasimamizi wa umoja wa mataifa wameripoti pia juu ya kuporwa mali katika eneo hilo.

Taarifa ya pamoja ya umoja wa mataifa na umoja wa Afrika imesema kuwa raia wanaoishi katika eno hilo wamelazimika kuuhama mji huo.

Hakuna taarifa zozote zinazo eleza kuhusu waliohusika na uvamizi huo na serikali ya mjini Khartoum bado haijatoa tamko lolote.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka umoja wa mataifa ni kwamba mji wa Haskanita ulio chini ya usimamizi wa serikali umeteketezwa vibaya isipokuwa nyumba chache tu zilizosalia.

Kiongozi wa kundi la waasi la SLA Suleiman Jamous amesema watu kadhaa wameuwawa na wakati huo huo ameilaumu serikali ya mjini Khartoum kwa kuhusika na tukio hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com