Mhamiaji wa kike apigwa risasi mpakani Misri | Habari za Ulimwengu | DW | 16.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mhamiaji wa kike apigwa risasi mpakani Misri

ISMAILIA:

Polisi kwenye mpaka wa Misri wamempiga risasi na kumuuwa mwanamke mmoja wa Kieritrea aliejaribu kujipenyeza Israel.Duru za polisi zinasema,mwanamke huyo alifyatuliwa risasi baada ya kupuuza amri ya kusimama.Murfit Meery aliekuwa na miaka 37 alijaribu kuingia Israel katika eneo la El Kuntilla,mashariki ya Rasi ya Sinai. Watoto wake wawili wa kike walio na umri wa miaka 8 na miaka10 wamezuiliwa na polisi.Sinai ni njia kuu inayotumiwa kusafirisha kimagendo watu wanaotafuta kazi au wanaoomba ukimbizi nchini Israel.Baadhi kubwa ya wahamiaji hao wanatoka nchi za Kiafrika.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com