Mgomo wa Lufthansa | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 22.02.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Mgomo wa Lufthansa

Mgomo huo wa siku nne ndio mkubwa kabisa katika historia ya Lufthansa.

Mgomo wa Marubani wa Lufthansa, waanza leo.

Mgomo wa Marubani wa Lufthansa, waanza leo.

Shirika la Ndege la Ujerumani, Lufthansa limeripoti kuwa marubani wake wameanza mgomo wao wa siku nne. Chama cha marubani hao, Cockpit, awali kilikuwa kimekubali kukutana na Mkuu wa shirika hilo la ndege, lakini kikakatalia mbali masharti ya awali yaliyowekwa na usimamizi wa shirika hilo. Marubani hao 4,000 wanaitisha nyongeza ya asili mia sita, pamoja na uhakika wa ajira.

Deutschland Verkehr Lufthansa Streik ab Montag Pilot

Marubani wataka nyongeza ya mishahara na uhakika wa ajira

Mgomo huo sasa unamanisha kutakuwa na msongamano wa abiria huku safari nyingi za ndege Barani Ulaya, zikicheleweshwa. Lufthansa inatarajiwa kufutilia mbali safari 800 za ndege kila siku, au theluthi mbili za ratiba yake. Waziri wa Usafiri wa Ujerumani Peter Ramsauer ameonya kuwa mgomo huo utaathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa Ujerumani na amejitolea kuwa mpatanishi wa mzozo huo wa malipo. Shirika hilo la ndege la Lufthansa, limesema mgomo huo ambao ndio mkubwa kabisa katika historia ya shirika hilo, utagharimu zaidi ya Euro milioni 65.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com